KIKOSI CHA SIMBA SC CHAENDELEA KUJINOA
Kikosi cha Simba SC kimefanya mazoezi leo asubuhi, mazoezi ya gym chini ya Kocha wa Viungo, Sbai Karim na kisha jioni kilifanya mazoezi yake uwanjani.
Kocha Sbai amejiunga na kikosi juzi na tayari ameanza kuwapa mazoezi ya
utimamu wa mwili ili kuwaweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Kikosi kinaendelea kufanya mazoezi kwa awamu mbili asubuhi na jioni huku
benchi la ufundi likiridhishwa na viwango vya wachezaji.
Tunatarajia kupata mechi nyingine ya kirafiki katika siku chache zijazo
ili kulipa nafasi benchi la ufundi chini ya Kocha Zoran Maki kuwasoma wachezaji
jinsi wanavyopokea mafunzo wanayowapa.
Hakuna maoni