Kikosi cha Azam SC kinaendelea na programu
kali ya mazoezi kambini mjini El Gouna, Misri.
Azam FC imetimiza
siku ya tatu ikiwa huko kambini, ambapo wachezaji wamekuwa wakifanyiswa mazoezi
ya nguvu ili kuhakikisha wanakuwa fiti.
Benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha
Mkuu, Abdihamid Moallin, limeshamaliza programu saba za mazoezi kwa siku tatu
za mwanzo.
Siku ya kwanza
juzi Jumamosi, wachezaji walifanyishwa mazoezi mara tatu, wakianzia na ile ya
uwanjani asubuhi kabla ya mchana kwenda ‘gym’ kuimarisha viungo na usiku
wakamalizia uwanjani tena.
AZAM SC YAENDELEA NA MAZOEZI MAKALI KAMBINI MISRI
Reviewed by Godfrey Kente
on
Julai 25, 2022
Rating: 5
Hakuna maoni