Google Ad

Breaking News

SUDAN KUSINI | IKIWA HUNA NG'OMBE WA KUTOSHA KAMA MAHARI, CHANCE YA KUPATA MKE KWAKO NI NDOGO MNO

HUKO Sudan Kusini, kulingana na tamaduni zao, kutoa idadi kubwa ya ng’ombe kwaajili ya kumposa binti ni jambo la kawaida, na ni heshima kubwa anapewa mposaji.

Hivyo kama huna ng'ombe wa kutosha kama mahari, uwezekano wako wa kuoa mke ni mdogo sana. Wanaume hutoa idadi kubwa ya ng'ombe ili kumchukua bibi harusi. Mwenye dau kubwa Zaidi kwa maana ya ng’ombe wengi Zaidi ndio mwenye kupewa mke.

Mnamo mwaka 2018, mwanamume mmoja katika nchi hiyo ya Sudan Kusini alivunja rekodi kwa kutoa ng'ombe 500, magari 2, baiskeli, na simu za mkononi zenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu kumi ($ 10,000) ambazo ni sawa na Shillingi za kitanzania takribani million 23.3 (23.3M) kwa familia ya bi harusi.



Hakuna maoni