MTOTO WA ALIYEKUWA RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE APATA AJALI MBAYA YA GARI
Mtoto wa aliyekuwa rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, Robert Tinotenda Junior, aliripotiwa kuhusika katika ajali ya kutisha baada ya gari lake la kifahari aina ya SUV kupinduka.
Kulingana na chapisho
la shirika la Habari la Bulawayo24, ajali hiyo ilitokea wakati gari lake aina
ya Range Rover Vogue lilipopinduka katika eneo la Nyanda za Juu Mashariki mwa
Zimbabwe.
Ajali ya Robert
Junior inaripotiwa kutokea eneo la Rwatsumbu kabla ya Watsomba, barabara ya
kutoka Mutare kuelekea Inyanga.
Chanzo cha ajali hiyo
bado hakijabainishwa.
Hata hivyo, mtoto wa
Rais huyo wa zamani inasemekana hajapata majeraha makubwa na kwa sasa yuko
hospitalini ambapo anaangaliwa.
Chanzo: Bulawayo24
Good site
JibuFuta