Google Ad

Breaking News

MASTAA 7 WA YANGA SC BADO HAWAJAFIKA KAMBINI

 

Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kuwa, mastaa 7 wa timu hiyo watajiunga na wenzao kambini mara baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa Julai 30, mwaka huu.

 

Kutokana na kuchelewa kwao, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, itabidi awasubiri kwa takribani wiki moja ndipo aweze kuendelea na mafunzo zaidi katika kukinoa kikosi hicho.

 

Wachezaji wa Yanga ambao wapo ndani ya Taifa Stars ni Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum, Farid Mussa na Salum Aboubakar.


Sababu ya wachezaji hao kutofika kambini hapo kwa wakati, ni kwamba wachezaji hao saba wapo katika kikosi cha Taifa Stars ambacho kilicheza mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN 2023 dhidi ya kikosi cha Somalia.

 


Hakuna maoni