Google Ad

Breaking News

PARIMATCH MDHAMINI RASMI WA MBEYA SC LIGI KUU TANZANIA BARA


KLABU ya soka, Mbeya City imepata udhamini kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri mitandaoni ya Parimatch.

Afisa Habari wa Parimatch, Ismail Mohamed, alisema kuwa kampuni ya  Parimatch inayoendesha shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni, leo tarehe Agosti 09 imeingia mkataba wa kuidhamini klabu ya Mbeya City inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.                                                    

Alisema kuwa hii mara ya pili kwa kampuni yao kudhamini Mbeya City, hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na Ushawishi na ndiyo  kurejea kwao kufanya udhamini. na kutoa vifaa vya michezo na kufanya ukarabati uwanja wa Sokoine.                                                                                      

Afisa Habari huyo Alisema kuwa Kampuni ya Parimatch moja ya jukumu lake katika michezo inakuwa   kuanzia ngazi ya chini mpaka Kimataifa.                                                                          

" Parimatch licha ya kuidhamini Mbeya City, ambayo inashiriki ligi Kuu Tanzania Bara, pia tunaidhamini Chelsea na Leicester City ambazo zinashiriki ligi ya Uingereza" Alisema Mohamed.                                                            

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema kuwa uongozi kwa niaba ya wachezaji na wanachama wa Timu, Wamefurahishwa na udhamini huo ambao utazidi kuipa chachu ya kufanya vizuri zaidi kwenye msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 15.                                                        

Alisema Parimatch waliwadhamini msimu wa 2020/21 hivyo kurudi kwao msimu huu, kumetokana na kuridhishwa kwao na udhamini huo uliopita.

Hakuna maoni