Google Ad

Breaking News

AISHI MANULA KUKOSA MECHI YA NGAO YA JAMII KESHO

MLINDAMLANGO nambari moja wa Simba SC, Aishi Manula ameripotiwa kuwa atakosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC utakaochezwa hapo kesho kutokana na kuwa bado hajawa fiti kiafya.

Manula alipata majeraha kwenye mchezo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Somalia uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

“Aishi Manula bado hajapona hivyo kuhusu kuanza kwake bado hataweza kuanza mchezo wa kesho labda ikitokea jambo lingine. Amesema kocha wa Simba SC Zoran Maki

“Lakini ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuweza kujiandaa vizuri ili kuweza kupata ushindi kwani tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkubwa,” amesema kocha.

Kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya St George,Manula hakuweza kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo na badala yake alianza Beno Kakolanya.

 

Hakuna maoni