CHELSEA WANAANGALIA UWEZEKANO WA KUIPIKU MANCHESTER CITY KATIKA KUMNASA BEKI WA UPANDE WA KUSHOTO MARC CUCURELLA
Chelsea wanatafuta dili la kumnunua beki wa kushoto wa Brighton, Marc Cucurella huku Manchester City ikiwa inamnyemelea pia.
Bei ya Brighton ya
Pauni Milioni 50 ilisababisha mazungumzo na Manchester City kukwama na vyanzo
vinasema Chelsea sasa wamefuatilia kwa kuhusu Mhispania huyo, wakiwa na lengo
la kumnasa.
Chelsea wapo sokoni kutafuta beki wa upande wa kushoto huku Marcos Alonso akielekea Barcelona.
Cucurella amewasilisha
ombi la uhamisho na akakosa mechi ya kirafiki ya Jumamosi thidi ya Espanyol.
Manchester City
walikuwa wametoa takriban pauni milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 26 na inasemekana kuna kero kwa upande wa Brighton kutokana na kutofikia
muafaka katika mazungumzo hadi sasa.
Hilo limefungua
milango kwa ofa za wapinzani na Chelsea ya Thomas Tuchel inavutiwa na mchezaji
ambaye alivutia macho wakati wa msimu wake wa kwanza kwenye Ligi ya Premia
msimu uliopita.
Hata hivyo,
inafikiriwa mchezaji wa zamani wa Barcelona Cucurella amekuwa akitamani sana
kucheza chini ya Pep Guardiola akiwa City, ambaye atalazimika kurejea na ofa
iliyoboreshwa ikiwa dili litakubaliwa.
Oleksandr Zinchenko,
ambaye alishiriki mara 28 katika mashindano yote kwa Guardiola msimu uliopita,
aliondoka Etihad na kujiunga na Mikel Arteta huko Arsenal mnamo Julai.
Hakuna maoni