YANGA IMETHIBITISHA KUFIKIA MAAMUZI YA KUACHANA NA WACHEZAJI WAKE WAWILI, CHICO USHINDI NA YACOUBA SOGNE
Yanga imethibitisha kufikia maamuzi ya kuachana na wachezaji wake wawili, Chico Ushindi na Yacouba Sogne baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Haji Manara, msemaji wa timu hiyo ya Yanga, Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ametoa taarifa hiyo mapema leo akizungumza na waandishi wa habari.
Haji Manara, akizungumza na waandishi wa Habari, pia alisema timu hiyo itaingia kambini kuanzia siku ya kesho Juni 20 kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao. Na wamechagua kukaa kambi maeneo ya Avic Town eneo la Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya..
Wachezaji wa kigeni wanaobaki Yanga sasa
ni beki Mkongo, Lomalisa Mutambala kutoka Sagrada Esperança ya Angola, viungo
Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kutoka ASEC Mimosa ya Ivory Coast, Mrundi, Gael
Bigiriamana kutoka Glentoran ya Ireland Kaskazini, winga Mghana, Bernard
Morrison kutoka Simba na mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya
Afrika Kusini.
Hao wanaungana na waliokuwepo tangu msimu uliopita, kipa wa kimataifa wa Mali, Djigui Diarra Wakongo, beki Djuma Shabani, viungo Yanick Bangala, Jesus Moloko, Mganda Khalid Aucho na weashambuliaji Wakongo pia, Heritier Makambo na Fiston Mayele kufanya idadi ya wachezaji 12 wa kigeni.
Yanga SC wanatarajia kuzindua kikosi chao kipya katika kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 6, kabla ya kukipiga na watani wao wa jadi, Simba SC katika mtanange wa Ngao ya Jamii, mtanange huo unatarajiwa kuchezwa Agosti 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni