Google Ad

Breaking News

DEAL DONE: AZAM FC YAMSAJILI BEKI MALICKOU NDOYE KUTOKA TEUNGUETH YA SENEGAL KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI.

 


Klabu ya Azam FC imehitimisha usajili wake kwa kumtambulisha beki wa kati, Malickou Ndoye mwenye umri wa miaka 22 kutoka Teungueth ya nchini kwao Senegal.

Usajili huo unafanya jumla yawachezaji 9 wapya, wengine ni kipa mkongwe Mcomoro raia wa Ufaransa, Ali Ahamada na viungo, James kutoka Ghana, Kipre Junior, Tape Edinho raia wa Ivory Coast, na Isah Ndala raia wa Nigeria.

Usajili mpya Wazawa ni, beki wa kulia, Nathaniel Chilambo kutoka Ruvu Shooting, viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union na Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji na kikosi kinaanza mazoezi leo jioni Chamazi.

" Maandalizi yataanza nyumbani kabla ya safari ya kwenda Misri.Tutaanza na kambi ya nyumbani siku ya Jumanne ambapo wachezaji waliopo pamoja na makocha wetu wapya watakua kwenye maandalizi ya msimu ujao.

Julai 22 tunatarajia kuanza safai ya kuelekea Misri na tutakua huko mpaka Mwezi Agosti. Tutatumia siko 20 na kurejea nyumbani kuendelea na maandalizi ya mechi zitakazokua zinatukabili" alisema Afisa habari wa Azam FC, Zakaria Thabit 




Hakuna maoni