MANARA AFUNGIWA MIAKA MIWILI NA FAINI MILIONI 20
Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili na faini ya Sh20 milioni kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam kati ya Yanga SC na Coastal Union iliyopigwa Jijini Arusha.
Manara amekutwa na hatia hiyo ya kumtishia na
kumdhalilisha Karia siku ya Jumamosi Julai 2, 2022 kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeid, Arusha wakati wa mechi ya fainali kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.
Akisoma hukumu hiyo, Lungu alisema katika mchezo huo,
Manara alitoa maneno yasiyofaa mbele ya Rais Karia huku akinukuu maneno hayo
kwa kusema " “Wewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa
lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya
chochote na huna cha kunifanya.”
Baada ya maneno hayo, Kamati imejiridhisha kumkuta
hatiani Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na
nje ya nchi na kumtodha faini ya Sh20 milioni adhabu ambayo inaanza rasmi
kuanzia leo Julai 21 mwaka 2022 japo anauwezo wa kukata rufaa.
Hakuna maoni