BAO LA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA SIMBA SC, PAPE SAKHO LAINGIA TATU BORA
Bao la kiungo
mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Pape Sakho alilofunga katika michuano ya
Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas limeingia tatu bora kwenye kinyang’anyiro
cha kutafuta bao bora la mwaka.
Sakho alifunga bao hilo Februari 13, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa
kwa acrobatic akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi, Shomari Kapombe.
Wachezaji ambao mabao yao yameingia tatu bora ni Gabadinho Mhango (Malawi & Orlando Pirates), Pape Ousmane Sakho (Senegal & Simba), Zouhair El Moutaraji (Morocco & Wydad Athletic Club). Tuzo za kutangaza bao bora ambazo mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura nyingi zitafanyika kesho saa 3 usiku Rabat nchini Morocco.
Hakuna maoni