YANGA YAJIGAMBA KUTWAA MAKOMBE YOTE MSIMU UJAO
Wawekezaji katika timu ya Yanga SC wametamba ya kuwa wanataka kubeba mataji yao, kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports ikiwa ni mkakati wao wa kutawala soka la Tanzania kiujumla.
Timu hiyo ys Yanga SC imetamba kwamba hakuna
wa kuizui hasa ukizingatia wamesaini mkataba mnono wa udhamini na Kampuni ya
SportPesa wa bilioni 12.3 huku wakiwa na uhakika wa kuingiza zaidi ya bilioni
moja kwa mwezi, ukiunganisha fedha za wadhamini wao wote, hiyo inawapa nguvu ya
kuendelea kujigamba kwamba watatwaa makombe yote msimu ujao.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Abbas
Tarimba amesema: “Tunajivunia kwa kufanikisha tukio letu muhimu la uzinduzi wa
jezi mpya ambazo bila shaka yoyote ndizo jezi bora zaidi kuiwahi kutengenezwa
nasi, hii ni sehemu ya maandalizi yetu ya kabla ya msimu unaokuja.
Kikosi hicho kwa sasa kinaendelea kujinoa
kule Avic Town, Kigamboni mkoani Dar es Salaam, wakiwa wanajiandaa na msimu ujao
wa ligi.
Hakuna maoni