TIMU NNE KUSHIRIKI NGAO YA JAMII KUANZIA MSIMU UJAO | BODI YA LIGI KUU TANZANIA
BODI ya Ligi
imefanya marekebisho ya kanuni kadhaa ikiwemo ya mchezo wa ngao ya Jamii sasa
kushirikisha timu nne.
Katika marekebisho hayo, timu tatu zilizomaliza nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara zitaungama na bingwa wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) katika michuano ya kuwania Ngao ya Jamii.
Na kama bingwa wa Azam
Sports Federation Cup ASFC atakuwa miongoni mwa timu zilizomaliza nafasi tatu
za juu kwenye Ligi Kuu, basi mshindi wa nne wa Ligi hiyo pia atashiriki Ngao ya
Jamii.
Hakuna maoni