Google Ad

Breaking News

WATU 28 WAFARIKI DUNIA WAKATI WENGINE 60 WAKIWA NA HALI MBAYA BAADA YA KUNYWA POMBE YA ILIYOTIWA METHANOL NCHINI INDIA.

 Takriban watu 28 wamefariki na wengine 60 kuugua kutokana na kunywa pombe iliyotiwa methanol ili kuongeza nguvu yake huko magharibi mwa India.

Vifo hivyo vimetokea katika wilaya za Ahmedabad na Botad katika jimbo la Gujarat, ambapo utengenezaji, uuzaji na unywaji wa pombe hiyo umepigwa marufuku.

"Kulikuwa na asilimia 98 ya methanoli katika pombe waliyokunywa, hiyo inamaanisha kuwa walikuwa wametumia methanoli pekee ambayo imeongeza idadi ya vifo," Bhavnagar Ashok Yadav, inspekta jenerali wa polisi, aliiambia Times of India.

Idara ya uhalifu ya jiji la Ahmedabad imemkamata mmiliki wa kemikali Jayesh Khavadiya kutoka Narol na washirika wake wanane kwa tuhuma za kusababisha vifo hivyo.

Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka zaidi baada ya wagonjwa kadhaa kufika katika hospitali ya kiraia ya Ahmedabad kwa matibabu.

Mkoa wa Gujarat umepiga marufuku unywaji pombe tangu 1960 kama heshima kwa Mahatma Gandhi, aliyeuawa mnamo 1948, lakini mamia ya wakaazi wamekufa kwa miongo kadhaa huku biashara haramu ya vileo ikiendelea kushamiri.

Pombe haramu pia imekuwa tasnia yenye faida kubwa kote India ambapo wafanyabiashara wa pombe hawalipi kodi na huuza kiasi kikubwa cha bidhaa zao kwa maskini kwa bei nafuu.

Polisi wa eneo hilo mara kwa mara hufumbia macho biashara ya vileo huku wafanyabiashara wa pombe wakilipa hongo ili kutekeleza uuzaji wao haramu katika vijiji hivyo, vyombo vya habari vya India viliripoti.

Mbunge wa Dhandhuka Rajesh Gohil pia alikuwa ameandikia mamlaka akiomba hatua dhidi kali dhidi ya walanguzi wa pombe katika eneo hilo zitekelezwe.

Mnamo mwaka wa 2019, takriban watu 133 walikufa baada ya kunywa pombe iliyochafuliwa katika matukio mawili tofauti katika jimbo la Assam kaskazini mashariki mwa India.

Waathiriwa wengi walikuwa wafanyikazi wa mashamba ya chai. Mwaka huo huo, watu wengine 80 walikufa kutokana na pombe iliyochafuliwa kaskazini mwa jimbo la Uttar Pradesh.

Mnamo 2020, watu wengine 120 walikufa baada ya kunywa pombe ya spiked katika jimbo la kaskazini la Punjab la India.








Hakuna maoni