TUZO YA GOLI BORA AFRIKA 2022 YAENDA KWA PAPE OUSMANE SAKHO
Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane
Sakho alilofunga dhidi ya ASEC kwenye mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho
Afrika limeshinda Tuzo ya Bora la Mwaka.
Wakati wa sherehe za utoaji wa Tuzo hizo za Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) usiku wa Alhamisi mjini Rabat nchini Morocco, Sakho ameshinda
dhidi ya Gabadinho Mhango wa Malawi nan Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji
wa Morocco na Wydad Athletic alioingia nao Fainali.
Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 tu akimalizia krosi ya beki
wa kulia, Shomari Kapombe katika ushindi wa 3-1 dhidi ASEC Mimosas ya
Februari 13, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao mengine ya Simba siku hiyo yalifungwa na Kapombe dakika ya 79 na winga
Mmalawi, Peter Banda dakika ya 81 akimalizia pasi ya Nahda, John Bocco, wkaati
bao pekee la ASEC lilifungwa na Stephane Aziz Ki 60 dakika ya 60.Senegal &
Simba)
Washindi wengine wa tuzo za CAF mwaka huu ni nyota wa Senegal
aliyejiunga na Bayern Munich akitokea Liverpool, Sadio Mane ambaye amebeba tena
Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mbele ya mwananchi mwenzake, kipa Edouard
Mendy wa Chelsea na Mohamed Salah wa Misri na Liverpool.
Ulikuwa usiku mzuri, baada ya Wasenegal wengine kubeba tuzo, Aliou Cisse
akichukuwa ya Kocha Bora wa Mwaka na Pape Matar Sarr wa Tottenham Hotspur
akiondoka na ya Mwanasoka Bora Chipukizi.
Asisat Oshoala wa Nigeria ameshinda kwa mara ya tano ya rekodi
Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike, huku Senegal ikishinda tuzo ya timu Bora ya
Taifa na Wydad Athletic ikibeba Tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume na Mamelodi
Sundowns Klabu Bora ya Wanawake.
WASHINDI WOTE TUZO ZA CAF BAO BORA LA MWAKA - Pape Ousmane Sakho
(Senegal & Simba)
MWANASOKA BORA WA MWAKA WA KIUME - Sadio Mane (Senegal and
Bayern Munich)
MWANASOKA BORA WA KIKE - Asisat Oshoala (Nigeria and FC
Barcelona)
MCHEZAJI BORA WA KIKE WA KLABU - Evelyn Badu (Ghana &
Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
MCHEZAJI BORA WA KIUME WA KLABU - Mohamed El Shenawy
(Egypt & Al Ahly)
MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIKE - Evelyn Badu (Ghana
& Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIUME - Pape Matar Sarr
(Senegal and Tottenham Hotspur)
KOCHA BORA WA MWAKA MWANAMKE - Desiree Ellis (Afrika
Kusini)
KOCHA BORA WA MWAKA MWANAUME - Aliou Cisse (Senegal)
KLABU BORA YA MWAKA YA WANAWAKE - Mamelodi Sundowns (South
Africa)
KLABU BORA YA MWAKA YA WANAUME - Wydad Athletic Club
(Morocco)
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME - Senegal
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME - Itapatikana baada ya
Fainali ya Afrika za Wanawake zinazoendelea Morocco
Hakuna maoni