SERIKALI YATENGA BILIONI 387. 73 KWAAJILI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAJI VIJIJINI
Serikali imetenga Shilingi Bilion 387.73 kwa ajili ya uwekezaji wa huduma ya maji maeneo ya vijijini ili kutatua changamoto inayowakabili wananchi.
Akizungumza leo jijini
Dodoma na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali
Mkurungezi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo amesema katika jitihada za
kuwapatia huduma muhimu wananchi hadi kufikia april mwaka huu hali ya
upatikanaji wa maji vijini ilikuwa asilimia 74.
Katika hatua nyingine
amesema katika mwaka huu wa fedha wanatarajia ongezeko la upatikanaji wa huduma
za maji kwa wananchi waishio vijijini kwa asilimia zaidi ya 6.
Msemaji Mkuu wa Serikali
Gerson Msigwa amesema Ruwasa wanajukumu la kuhakikisha wanamtua mama Ndoo
kichwani.
Inatarajiwa kuwa Ifikapo
mwaka 2025 Ruwasa itafikia zaidi ya asilimia 85 ya utoaji wa huduma ya maji kwa
wananch waishio vijijini.
Hakuna maoni