MWANAMUZIKI WA POP RICKY MARTIN ASHTAKIWA NA MPWA WAKE AKIMTUHUMU KUMDHALILISHA KIJINSIA
Wakili wa mwimbaji nyota wa muziki wa pop Ricky Martin amekanusha vikali madai kwamba mwimbaji huyo alimdhalilisha mpwa wake, na kuyaita madai hayo "sio tu ya ukweli" bali "ya kuchukiza".
Martin alipewa
agizo la zuio “restraining order” huko Puerto Rico mapema Julai. Agizo hilo
lilitaja shutuma za unyanyasaji wa kijinsia.
Siku ya Ijumaa,
tovuti ya burudani ya TMZ iliripoti kwamba kakake mwimbaji huyo, Eric Martin,
alimtambua mwathiriwa huyo kuwa mpwa wa Martin mwenye umri wa miaka 21. TMZ
ilinukuu tovuti ya habari ya Uhispania ya Marca. Wakili Martin Singer hata
hivyo alidai kwamba mpwa wa Martin "anapambana na changamoto kubwa za afya
ya akili".
Katika taarifa
kwa Variety, Mwimbaji alisema: "Ricky Martin, bila shaka, hajawahi - na
hatawahi - kushiriki katika aina yoyote ya uhusiano wa kimapenzi na mpwa wake.
Wazo sio tu sio kweli, ni chukizo. Sote tunatumai kuwa mtu huyu atapata msaada
anaohitaji haraka sana. Lakini, zaidi ya yote, tunatazamia kesi hii mbaya
itupiliwe mbali mara tu jaji atakapoanza kuangalia ukweli.”
Wakati agizo la
zuio lilipowasilishwa Julai 2, mwombaji alikuwa hajatambuliwa. Chombo cha
habari cha Puerto Rican El Vocero kiliripoti kwamba hatua hiyo inadaiwa kutoka
kwa mtu ambaye Martin alikuwa amechumbiana nae kwa miezi saba. Wakati huo,
mwombaji alisema Martin alikana kutengana na amekuwa akionekana karibu na
nyumba yao mara kadhaa.
Martin, kwa mujibu wa TMZ, atafikishwa mahakamani Julai 21, wakati jaji ataamua iwapo zuio hilo linafaa kubaki pale au kusitishwa.
Hakuna maoni