MIILI YA WATU 20 WALIOKUTWA WAMEFARIKI JANGWANI NCHINI LIBYA, CHANZO CHATAJWA KUWA NI KUKOSA MAJI (KIU)
Miili ya Takribani watu 20 waliokutwa wakiwa wamefariki katika jangwa nchini Libya, sababu imetajwa kuwa ni kiu baada kukosa maji kwa muda mrefu huku kukiwa na wasiwasi kuwa watu hao yawezekana walikuwa wamepotea njia na kukosa msaada kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari AFP, miili hiyo iligunduliwa na Dereva wa magari ya masafa marefu na pia inasadikika ya kuwa miili hiyo imegunduliwa baada ya watu hao kupotea kwa muda wa zaidi ya wikli mbili
Waokoaji wakiendelea kuokoa miili ya watu hao
walifariki Jangwani nchini Libya
Dereva huyo anadaiwa kuigundua miili hiyo wakati anasafiri kukatiza Jangwa hilo umbali wa kilomita 320 Kusini Magharibi mwa Kufra na Kilomita 120 kutoka mpaka wa Chad. “Dereva alipotea na tunaamini kundi lilipotea na kufia jangwani siku 14 zilizopita tangu mara ya mwisho yafanyike mawasiliano ya simu ni Juni 13.” Alisema Afisa wa Ambulance wa Kufra, Ibrahim Belhasan kupitia njia ya simu.
Miili miwili kati ya miili ishirini ilikuwa ni ya raia wa Libya, iliyobaki inaaminika kuwa ni ya raia wa Chad ambao walikuwa wanavuka Jangwa kuingia nchini Libya.
Miili hiyo iligundulika mnamo June 29, 2022
Hakuna maoni